TANGAZO


Thursday, September 4, 2014

Wito watolewa silaha zisiuzwe Sudan Kusini


Mashirika ya kutoa misaada yametoa wito wa kutaka kusitishwa kuuzwa kwa silaha kwa Sudan Kusini ambapo mapigano kati ya serikali na waasi yamewalazimu zaidi ya watu nusu milioni kukimbia makwao.
Muungano huo wa zaidi ya mashirika 30 unasema kuwa pande hizo zote zinatumia silaha kutoka nje kutekeleza uhalifu wa kivita.
Mashirika hayo sasa yanaitaka IGAD na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupiga marufuku uuzaji wa silaha kwa udan kusini.
Mwezi Julai ripoti zilisema kuwa maelfu ya tani ya bunduki, maguruneti na riasi vilisafirishjwa kwenda nchini humo kutoka China.
Marekani na Muungano wa ulaya tayari wametangaza marufuku hiyo.

No comments:

Post a Comment