Kundi la Sudan Kusini la SPLA/M lililojitenga na kuongozwa na aliekuwa makamu rais wa Sudan Kusini Dr Riak Machar linasema halitambui mapatano ya mjini Addis Ababa ambayo yalikuwa ya kugawana madaraka na rais Salvar Kiir.
Pia kundi hilo sasa limebadili msimamo wake wa hapo awali wa kulitaka jeshi la Uganda la UPDF kuondoka Sudan Kusini na badala yake kulipongeza kwa kazi linayoifanya huko.
Jeshi la Uganda limekua likiisadia serikali ya Juba kukabiliana na mashambaulizi ya wapiganaji wa Dr Riak Machar.Kundi hili limefungua ofisi yao mjini Kampala Uganda.
Kundi linaloongozwa na Dr Rieck Machar lasema linafungua sura mpya ya uhusiano na utawala wa Kampala ambao unausadia utawala wa Juba chini ya rais Salvar Kiir.
Serikali ya Sudan Kusini imekuwa inapigana vita dhidi ya wapiganaji walioasi kutoka kwa serikali hiyo wakiiunga mkono Dr Riek Machar ikiungwa mkono na wanajeshi wa Uganda na hivyo Machar kuuona utawala wa kampala kama adui.
Lakini sasa kundi la Machar laonekana kubadili kauli hiyo na hivyo kunyoosha mkono wa urafiki kwa kufungua ofisi yao mjini Kampala.
Hayo yamebainishwa na mmoja wa kundi wa wanakundi hilo -David Otim- ambae anaedai kuwa kateuliwa kuwa mkuu wa ujumbe huo nchini Uganda.
Amewaambia waandishi habari mjini Kampala kuwa kundi lao sasa linaunga mkono jeshi la Uganda la UPDF kuendelea kukaa Sudan Kusini na kutoa sababu.
Ni kutokana na matokeo ya makubaliaono ya mjini Kampala.
Na tunajua kuwa sasbabu kwa nini UPDF iko huko kuna ombwe Fulani.
Lazima tukubali hilo na vilevile kuna masuala yaliyotajwa kuwepo kwa makundi hasimu kama vile LRA na mengine kwa hivyo ni lazima tukubali kwani tukikubali UPDF kuondoka Sudan Kusini itakuwa kuna ombwe na kutokana na hilo tumekubali libaki kulinda watu na mali lakini kwa muda tukisubiri IGAD kutuma kikosi kamili na wala sio kushiriki katika mapigano.
Ufungunzi wa ofisi ya kundi hilo mjini kampala unakuja wakati kikao cha sita cha awamu ya pili ya mkutano wa kutafuta amani nchini Sudan Kusini wa shirika la IGAD kikianza mjini Addis Ababa ambapo inasemekana washiriki wamekubali hati jaribio ya makubaliano ya utawala wa mpito kuelekea ufumbuzi wa mgogoro wa Sudan Kusini.
Miongoni mwa mengine hati hiyo inapendekeza ni pamoja na ugawanaji wa madaraka kati ya mahasimu wawili yaani rais Salavra Kiir kubali kama rais na Dr Riek Machar kuwa waziri mkuu ambae anateuliwa na rais.
Lakini kundi la Dr Machar katika mkutano na waandishi habari wa Kampala wamepuuzia mbali itifaki hiyo.
''Sisi katika SPLM/ A tumenuiya kufuata mchakato wa kuleta amani ambao unapangwa na IGAD lakini hatutambui hati ya itifaki ya viongozi sita wa IGAD walioitoa juzi ambayo inampendelea Generali Salvar Kiir na serikali yake.''
Kundi hilo linasema kuwa linachukulia tu hati hiyo kama sehemu ya muendelezo wa majadiliano na pande zote husika katika mgororo huo na wala sio uamuzi wa mwisho.
Aidha afisa huyo akiambatana na Prof Oyet Nathaniel Pierino ,mwenyekiti wa kamati ya SPLM/A inayohusika na uhamasishi, wamesem akuwa wako tayari kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC ikiwa wataombwa kufanya hivyo kujibu madai ya uhalifu wa kivita wakati wa mapigano kati ya wapaiganaji wao na wanajeshi wa serikali ya Juba hivi majuzi.
No comments:
Post a Comment