TANGAZO


Sunday, September 21, 2014

Simba yavutwa mkia na Coastal Union


Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Wagosi wa kaya (Coastal Union), wakati zilipopambana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zimetoka suluhu kwa kufungana mabao 2-2. Simba ndiyo iliyotangulia kwa kuongoza kwa mabao 2-0 kwa kipindi chote kwa kwanza. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Wagosi wa kaya (Coastal Union) ya Tanga, wakati zilipopambana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Coastal Union na Simba wakiwania mpira karibu na lango la Simba, wakati wa mchezo huo leo.
Mashabiki wa timu ya Simba, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya Wagosi wa kaya (Coastal Union), Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. 
Mchezaji Yayo Lutimba wa Coastal Union (kushoto), akiruka juu kuwania mpira na Raphael Kiongera wa Simba wakati wa mchezo huo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Rama Salum wa Coastal Union (kushoto), akiondoka na mpira huku akifuatwa Emmanuel Okwi wa Simba.
Emmanuel Okwi (kulia) wa Simba, akiwania mpira na Tumba Lui wa Coastal Union.
Mashabiki wa timu ya Coastal Union ya Tanga, wakifurahia bao la kwanza la timu hiyo, wakati wa mchezo dhidi ya Simba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Coastal Union, wakicheza na kuimba wakati timu yao ilipoanza kufunga mabao ya kusawazisha dhidi ya Simba iliyokuwa imetangulia kushinda mabao 2-0 hadi kinamalizika kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Emmanuel Okwi wa Simba (mbele), akikimbia na mpira huku akifuatwa na Nahodha wa Coastal Union, Hamis Kibacha. 
Emmanuel Okwi wa Simba (mbele), akimtoka Nahodha wa timu ya Coastal Union, ya Tanga, Hamis Kibacha.
Raphael kiongera wa Simba (katikati), akiwaniakumtoka Abdallah Mfuko wa Coastal Union.
Raphael kiongera wa Simba (kushoto), akijaribu kutaka kumpiga chenga Hamis Kibacha wa Coastal Union.
Raphael kiongera wa Simba (kushoto), akijaribu kuutuliza mpira kabla ya kuupiga huku akifuatwa kwa karibu na Sabri Rashid wa  Coastal Union.
Wachezaji wa Coastal union wakishangilia bao lao la pili la kusawazisha na kumaliza mchezo huo kwa kufungana mabao 2-2.
Mashabiki wa Coastal Union, wakishangilia bao la pili la kusawazisha baada ya Simba kutangulia kushinda na kuongoza kwa mabao 2-0 hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Ubao wa matangazo ukionesha timu hizo kuwa mabao 2-2 baada ya Coastal Union kusawazisha mabao yote mawili ilyokuwa imeshafungwa na timu ya Simba katika mchezo huo.
Raphaele Kiongera wa Simba akiuangalia mpira aliokuwa akiukimbilia baada ya kudakwa na golkipa Shaaban Kado wa Coastal Union.
Raphaele Kiongera (12) wa Simba akiwa amelala chini na golkipa Shaaban Kado wa Coastal Union, baada ya kugongana wakati wakiruka juu kuwania mpira..
Shaaban Kisiga (katikati), akikimbilia mpira huku akifuatwa na Abdallah Mfuko wa Coastal union katika mchezo huo.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba (katikati), akitafuta mbinu ya kuwatoka Ayoub Yahya (kushoto) na Sabri Rashid wa Coastal Union.
Ramadhan Singano 'Messi' wa Simba (katikati), akipambana na Ayoub Yahya (kushoto) na Sabri Rashid wa Coastal Union.
Wachezaji wa Simba wakitoka nje ya Uwanja baada ya mchezo kati ya timu hiyo dhidi ya Coastal Union kuisha kwa kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.
Wachezaji wa Simba wakitoka nje ya Uwanja baada ya mchezo kati ya timu hiyo na Coastal Union kumalizika na kufungana mabao mawili kwa mawili. 
Jopo la Makocha wa Simba wakitoka nje ya Uwanja baada ya mchezo wa timu yao ya Simba dhidi ya Coastal union kumalizika kwa kufungana mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment