TANGAZO


Saturday, September 6, 2014

Serikali yatumia zaidi ya Bilioni 16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (The Law School of Tanzania

 
Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi akiwaeleza jambo waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole.
Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole akiwaleza waandishi wa habari lengo la uanzishwaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ikiwa ni kuwaongezea ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kutoa huduma bora na yenye tija ka wananchi, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
Mwanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bw. Edwin Rwekaza akiwaleza waaandishi wa habari kuhusu msisitizo unaotolewa na Taasisi hiyo katika mafunzo kwa vitendo ili kuwaongezea ujuzi katika utekelazaji wa majukumu pindi watakapo hitimu, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
 Mhadhiri wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Emil Lukiko akiwaeleza jambo waandishi wa habari (Hawapo pichani) , wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
 Mkuu wa Kitengo cha Mitihani wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Ipyana Mwaikambo akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani), Kuhusu idadi ya wanafunzi waliodahiliwa toka Taasisi hiyo imeanzishwa ambapo alisema zaidi ya wanafunzi 4000 wameshadahiliwa mpaka sasa, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
 Ofisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole akiwaleza waandishi wa habari lengo la uanzishwaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ikiwa ni kuwaongezea ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kutoa huduma bora na yenye tija ka wananchi.
 Jengo la Kufundishia(Teaching Block) katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) lenye vyumba 2 vya mihadhara(lecture rooms) vyenye uwezo wa kuingiza wanafunzi 460 kila chumba, vyumba 72 vya semina.

Jengo la Mahakama ya kujifunzia (Teaching Court) lililopo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) litalofungwa Video Link ili wanafunzi waweze kujionea moja kwa moja namna kesi zinavyoendeshwa.
 Muonekano wa ndani wa Chumba cha Mahakama katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School)
10- Muonekano wa ndani wa chumba mihadhara(lecture rooms)
(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO)
Muonekano wa ndani wa chumba mihadhara(lecture rooms)
(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO)
Na Frank Mvungi-Maelezo 
SERIKALI  itumia zaidi ya  Bilioni  16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (the law school of Tanzania).
Hayo yamesemwa  leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika taasisi hiyo iliyolenga kuona hatua iliyofikiwa tangu kuanza kwa ujenzi wake mwaka 2010.
“Baada ya kukamilika kwa ujenzi huu mwaka 2013 uendeshaji wa mafunzo ulihama kutoka  chuo kikuu cha Dar es salaam na kuanza kutumika kwa majengo haya ya kisasa yaliyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na sheria”
Akifafanua Ngole amesema ujenzi huo umehusisha ujenzi wa Mahakama ya mafunzo, (Teaching Court) vyumba vya madarasa (leacture theartres),Maktaba ya Kisasa (Library) Jengo la Utawala ( Admistration block) Mgahawa na nyumba za watumishi.
Pia Ngole alitoa wito kwa wanasheria wote wanaohitimu katika Taasisi hiyo kuwa tayari kutoa huduma popote pale nchini Tanzania kwa kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kuanzisha Taasisi hiyo ili iwanufaishe wananchi wote.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mitihani  bw. Ipyana Mwaikambo alisema Taasisi hiyo imeshadahili wanafunzi zaidi ya 4000 toka kuanzishwa kwake mwaka 2008 hadi sasa.
Naye Mmoja wa wanafunzi wa Taasisi hiyo Bw. Edwin Rweykaza amesema Taasisi hiyo inatoa msisitizo katika mafunzo ya vitendo na kuwajengea uwezo wa kutimiza majukumu yao mara baada ya kuhitimu.
Kuhusu maadili Rweykaza alibainisha kuwa  ni swala linalopewa kipaumbele kwa wanafunzi wote wanaojiunga na Taasisi hiyo.
Serikali imetimiza  ndoto ya miaka mingi ya kujenga majengo ya kisasa ya Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (The law school of Tanzania) inayotoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili kwa lengo la kuongeza stadi na ujuzi wa wanasheria hao katika kuwahudumia wananchi.

No comments:

Post a Comment