
Mwathiriwa wa ugonjwa wa Ebola abebwa na maafisa wa afya
Mshauri wa rais wa Sierra
Leone ,moja ya taifa la afrika magharibi ambalo limeathiriwa vibaya na
ugonjwa wa Ebola amesema kuwa serikali itaanzisha mpango wa siku nne wa
kuwatenga raia ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Mpango huo utaanza tarehe 18 mwezi
Septemba.Mshauri huyo Ibrahim Ben Kargabo amesema kuwa hatua hiyo
itawawezesha maafisa wa afya kuwatafuta wagonjwa wa Ebola,na kuelezea
kuwa ni njia mojawapo kusitisha ueneaji wa ugonjwa huo nchini Sierra
Leone kabisa.Amesema kuwa zaidi ya watu elfu ishirini watapelekwa katika makaazi ili kuhakikisha kuwa raia wanasalia majumbani mwao.
Tayari baadhi ya miji karibu na mpaka wa Guinea imetengwa.
No comments:
Post a Comment