*Lapendekeza Makamu wa tatu wa Rais
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge, akiwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati wa kikao cha arobaini na mbili cha bunge hilo leo, mjini Dodoma.
Na Mwandishi wetu_MAELEZO_Dodoma
Bunge Maalum la Katiba limependekeza
muundo wa uongozi wa Serikali utakuwa na Makamu watatu wa Rais wa Jamhuri
Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo, imetolewa leo mjini
Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Andrew Chenge wakati akiwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa
wakati wa kikao cha arobaini na mbili cha Bunge hilo.
Amesema kuwa katika mapendekezo hayo
mgombea mwenza ndio atabaki kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, na kwa upande
wa Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa
tatu wa Rais.
Amesema kuwa Kamati hiyo ya uandishi
imeona ni busara mgombea mwenza kuendelea kuwa Makamu wa Rais kwa kuwa
itakuwa rahisi kwake kukaimu uongozi kama itatokea bahati mbaya Rais
aliyemadarakani hatakuwepo kwa namna moja au nyingine kwani
ataendeleza ilani za mwenzake kuliko atakavyokuwa wa kutoka Zanzibar kama
kutakuwa na vyama viwili tofauti vinatawala.
Kwa upande wa Rais wa Zanzibar kuwa
Makamu wa pili , Chenge amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha muungano
kwani kiongozi huyo ni kiungo muhimu katika kudumisha Muungano.
"Suala la Rais wa Zanzibar kuwa Makamu ni la msingi kwa kuwa ni kiungo muhimu ikizingatia historia ya nchi tangu mwaka 1964 muungano ulipoasisiwa ilikuwa hivyo hadi mfumo wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1992,” alisema Mhe. Chenge huku akiongeza kuwa anakuwa hivyo kwa nafasi yake.
Ameongeza kuwa Waziri Mkuu anakuwa
Makamu wa Tatu kwa mujibu wa Cheo chake.
No comments:
Post a Comment