Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd, akikanusha taarifa kuhusu kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, mjini Dodoma leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd, akisoma taarifa ya kukanusha kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, mjini Dodoma leo.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akieleza jambo, wakati wa mkutano na waandishi kuhusu kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akifafanua jambo, wakati wa mkutano na waandishi kuhusu kukanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo, lililodai kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, mjini Dodoma leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo wakifuatilia kwa makini taarifa zilizokuwa zikitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif
Ali Idd amekanusha madai mbalimbali yaliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la
Jumatano 24 Septemba, 2014 ambalo liliandika kuwa ‘Siri zavuja za AG Zanzibar
kujiuzulu’.
Akikanush taarifa hizo, Mhe. Balozi Idd amesema kuwa
Mhe. Othman alitakiwa ashiriki katika kamati kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Zanzibar lakini kutokuwepo kwake katika
Kamati sio kikwazo cha kupatikana kwa Katiba, kwani waliokuwepo ndani ya kamati
kwa upande wa Zanzibar walitosheleza kuiwakilisha Zanzibar kikamilifu.
Mhe. Balozi Idd alifafanua kuwa Mjumbe kuchaguliwa
katika kamati na kukataa kuhudhuria ni maamuzi yake binafsi na hakuna lazima ya
mjumbe kuchaguliwa kuingia katika kamati fulani ikawa ndiyo kifungo licha ya
kwamba atakuwa na wajibu wa kuendelea kufanya kazi katika kamati hiyo hadi
mwisho.
“Sisi kama Serikali tunakanusha suala la sintofahamu
iliyoandikwa na gazeti hilo ambayo imedai kwamba Viongozi wa juu wa CCM
walikutana kwa dharura na kuazimia kumfukuzwa kazi kwa Mwanasheria huyo kwa
kile walichodai amekisaliti Chama”, alisema Balozi Idd.
Akizungumzia juu ya uwepo wa hoja 17 ambazo zilitakiwa
kuwasilishwa na Mwanasheria Mkuu huyo, aisema kwamba Mwanasheria hiyo tayari
alishaziwasilisha n azote ziliingizwa katika Rasimu ya Katiba isipokuwa Hoja
Nne ambazo bado zinafanyiwa kazi.
Aidha ameongeza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
hatakiwi kuwa muumini wa Chama chochote cha siasa na ndiyo maana hata vikao vya
chama hatakiwi kuhudhuria, hivyo Mwanasheria huyo wa Serikali si mteule wa
chama bali ni mteule wa Mhe. Rais was Zanzibar na ndiyo mwenye maaumuzi ya
kumuondoa ama kutomuondoa.
Akizungumzia kuhusu tuhuma za kufanyika kwa kikao cha
Mawaziri wote wa SMZ wakiongozwa na Dkt. Shein ili kuelezwa taarifa ya
Mwanasheria huyo juu ya masuala 17 aliyotaka yaingizwe katika Rasimu ya Katiba
alikanusha kuwa, suala hilo sio kweli kwani baadhi ya waandishi wa habari
hawafahamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina Mfumo wa Umoja wa Kitaifa
ambao umeundwa na CCM na CUF.
“Kama inavyoeleweka CUF hawamo katika Bunge Maalum la
Katiba, sasa itakuwaje washiriki kuchangia masuala ambayo wao kama sehemu ya
UKAWA hawakubaliani na kuendelea kwa Bunge hilo?”, alihoji Balozi Idd.
Mhe. Balozi Idd amevitaka Vyombo vya habari kuandika
habari zenye ukweli na amewataka kupuuzia uvumi unaoenea katika mitandao ya
kijamii kuhusu vitisho vitolewavyo na baadhi ya watu wenye nia ya kuwatisha
baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwani vyombo vya dola linafahamu juu ya uwepo
wa vitisho hivyo na inavifanyia kazi.
No comments:
Post a Comment