Marehemu Idd Pandu Hassan wakati wa uhai wake. |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na ndugu wa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, wakati alipofika kuwapa pole wafiwa nyumbani kwa marehemu Magomeni, Mjini Zanzibar leo, kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
Baadhi ya akina mama walioshiriki katika mazishi ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu Iddi Pandu Hassan, wakiwa nyumbani kwake Magomeni, Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa nnne kulia), akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume wakijumuika na Waisalmu katika kumswalia Marehemu, aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Iddi Pandu Hassan katika Msikiti wa Mchekeni, Magomeni Mjini Zanzibar leo na kuzikwa kijijini kwao Makunduchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk. Mohamed Gharib Bilali walioungana na wananchi mbalimbali katika maziko ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Iddi Pandu Hassan aliyezikwa kijijini kwao, Kipunguni Makunduchi leo. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu)
No comments:
Post a Comment