Real Madrid na Atletico Madrid zilitoka sare ya bao moja katika mechi ya mkondo wa kwanza wa kuwania ubingwa wa Super Cup.
Mshambulizi nyota wa Colombia James Rodriguez,
aliyejiunga na Real hivi majuzi baada ya kushinda “Golden Boot” katika
kombe la dunia, ndiye aliifungia timu yake bao moja (80’), lakini Raul
Garcia aliisawazisha Atletico Madrid.Mchezaji wa Real Cristiano Ronaldo, ambaye pia ni mchezaji bora wa mwaka ulimwenguni, hakushiriki katika kipindi cha pili cha mchezo huo, baada ya kujeruhiwa.
Rodriguez, aliyekuwa mshambuliaji wa Monaco, alichukua nafasi Cristiano, na kung’aa kwa mara ya kwanza katika uga wa Bernabeu.
- Kuzaliwa: Cucuta, Colombia, 12 July, 1991
- Alikuwa mchezaji akiwa Colombia na Argentina, kabla ya kutia saini mkataba na Porto 2010, na kufunga mabao 32 katika mechi 105 na kushinda taji tatu za Ureno, na ligi ya Uropa.
- Alijiunga na Monaco 2013, na kufunga mara 10 katika mechi 38
- Alifungia Colombia mara sita katika kombe la Dunia na kushinda “Golden Boot.”
Gareth Bale alifanya mashambulizi mawili makali dhidi ya Atletico, huku mlinda lango Miguel Angel Moya akiokoa kufuatia jaribio la kwanza na kumakinika kwa mara ya pili baada ya Gareth kumpa jaribio la mkwaju mkali.
Japo Moya hakuudaka mpira baada ya mkwaju wa Gareth, Toni Kroos wa Real hakuweza kuurejesha mpira wavuni.
Mkwaju wa Karim Benzema ulizuiwa lakini mpira ukamuangukia Rodriguez aliyeusukuma wavuni.
Real walionekana kushikilia usukani baada ya bao la kwanza, huku wakielekea kuchuana tena dhidi ya vijana wa Vicente Calderon, lakini Atletico, kwa mara nyingine, ilidhihirisha kuwa wachezaji wake hawakati tamaa kwa urahisi.
Atletico ambayo haikushindwa msimu uliopita na Real wala Barcelona katika Super Cup, iling’aa tena ikichuana na Real baada ya Garcia kusawazisha alipofaulu kumfunga mlinda lango wa Real Iker Casillas.
Hata hivyo, Atletico imewapoteza Diego Costa, Filipe Luis, David Villa na Thibaut Courtois tangu kushindwa na Real katika fainali ya ligi ya mabingwa msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment