TANGAZO


Wednesday, August 20, 2014

Israel yamlenga kiongozi wa Hamas





Mgogoro wa Gaza

Kikundi cha Hamas kimesema mke na mtoto wa kamanda wake wa kijeshi, Mohammed Deif, wameuawa katika shambulio la anga la Israel katika Ukanda wa Gaza.
Wapalestina wapatao 11 wameuawa tangu mapigano mapya yazuke Jumanne, huku kila upande ukiulaumu upande mwingine kwa kushindwa kuendelea kwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakifanyika mjini Cairo, Misri.
Jeshi la Israel limesema limefanya mashambulio 60 ya anga ili kukabiliana na makombora 80 yaliyorushwa na Hamas katika ardhi ya Israel.
Mapigano makali yaliyodumu kwa wiki sita yamesababisha watu 2,100 kuuawa.
Misri imeelezea masikitiko yake mwishoni mwa siku 10 za utulivu na kusema kuwa itaendelea kujaribu kupata ufumbuzi wa kudumu wa kusitisha mapigano kati ya Israel na Wapalestina.
Inaaminika kuwa shambulio la anga katika nyumba moja katika mji wa Gaza Jumanne ambalo limemuua mke wa Mohammed Deif na mtoto wao mdogo wa kiume lilidhamiriwa kumuua mpiganaji mwenyewe, anaripoti mwandishi wa habari wa BBC Kevin Connolly mjini Jerusalem.
Mashambulio mengi ya anga ya Israel yameripotiwa kote katika Ukanda wa Gaza baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuvunjika.
Wakiilaumu Israel kwa kufungua "lango la jehanamu", Hamas walifyatua makombora kuelekea miji ya Tel Aviv na Jerusalem


Mgogoro wa Gaza kati ya Israel na Wapalestina
Mamia ya Maelfu ya Wapalestina huko Gaza wameyakimbia makazi yao kutokana na mgogoro unaoendelea.
Vifaru vya jeshi la Israeli vimebakia katika mpaka na Gaza. Kamnda wa tawi la kijeshi la chama cha Hamas la Brigedi za Izz al-Din al-Qassam, amenusurika katika majaribio kadha ya Israel ya kumuua na inaaminika amebaki na ulemavu mkubwa wa viungo.
Waziri wa mambo ya ndani wa Israel Gideon Saar amesema shambulio hilo lilistahili kwa sababu Mohammed Deif "binafsi alihusika" kwa vifo vingi vilivyotokea.
Waziri wa sayansi wa Israel Yaakov Perry, na mkuu wa zamani wa usalama, amesema "alishawishika kuamini kuwa kama habari za kiinteljensia zingebainisha kuwa Mohammed Deif hakuwa nyumbani, kwa hiyo tusingeshambulia nyumba hiyo".
Habari za awali zinasema mwili wa mtu wa tatu ulivutwa kutoka kifusi cha nyumba, lakini madaktari wanasema ni watu wawili tu waliofariki dunia.
Shambulio lingine la anga mapema Jumatano limeua watu saba, akiwemo mama mjamzito na watoto watatu, katika wa mji wa Deir al-Balah katikati ya Gaza, msemaji wa huduma za dharura Ashraf al-Qudra ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP.

No comments:

Post a Comment