TANGAZO


Monday, July 7, 2014

Utata kuhusu kanda ya Pistorius

Wakili wa Pistorius analalamika kuwa kanda hiyo ya video imefichuliwa kisiri
Kituo kimoja cha televisheini nchini Australia kilichoonyesha kanda ya video ya mwanariadha Oscar Pistorius akisimulia kilichotokea hadi akamuua mpenzi wake, imejitetea kwa kupeperusha kanda hiyo.
Channel 7 imesema kuwa iliipata kanda hiyo kwa njia halali.
Utetezi unatafakari kuhusu kumaliza kutoa ushahidi.Kanda hiyo ilipeperushwa tu kwa stesheni hiyo Jumapili na kinamuonyesha Pistorius akipiga mayowe na kukimbia kwa miguu yake bandia huku akishika bunduki.
Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius imeanza kusikilizwa tena leo, huku picha za video zinazomuonyesha mwanariadha huyo akisimulia alivyomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp zikiwa zimetolewa.
Wakili wa Pistorius amevilaumu vyombo vya habari vya Australia kwa kurusha picha hizo za video kwa madai kuwa zilipatikana kinyume cha sheria.
Mwandishi wa BBC nchini Afrika kusini anasema huenda ushahidi ulioonyeshwa kwenye picha hizo ukatumika katika mashitaka hayo ya Pistorius.
Picha hizo zimeonyeshwa jana katika runinga moja nchini Austarilia, msemaji wa Pistorius amesema kuwa picha hizo zilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi japo kuwa ilikuwa katika mfumo ambao ni kinyume cha sheria.
"Kwa upande wa familia kurushwa kwa picha hizo ni kama kuingilia uhuru binafsi” anasema msemaji huyo. Hata hivyo picha hizo hazijawahi onyeshwa nchini Afrika Kusini ambako ndiko kesi hiyo imekuwa ikiendeshwa.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding aliyepo Afrika Kusini anasema haifahamiki mara moja kwanini picha hizo hazikutumika kama kielezo katika kesi ya Pistorius.
Pistorius mwenyewe ameendelea kusisitiza kuwa alimuua mpenzi wake kwa bahati mbaya akidhani kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi.
Mwanariadha huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Steenkamp kwa takribani miaka mitatu kabla ya mauaji hayo.

No comments:

Post a Comment