TANGAZO


Tuesday, July 22, 2014

Rais Dkt. Jakaya Kikwete aendelea na ziara Namtumbo


D92A7268 
Mtoto Gloria Fusi mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Utwango wilayani Namtumbo akiandika jina lake katika Notebook ya Mama Salma Kikwete wakati Rais Kikwete aliposimama katika kijiji cha Utwango kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mjini Namtumbo akitokea Songea mjini. Mtoto Gloria alimsalimia Mama Kikwete kwa uchangamfu na ndipo Mama Salma alipomuuliza kama anajua kuandika jina lake na hivyo kumpatia notebook yake na mtoto huyo bila kusita aliandika vizuri jina lake.
D92A8180 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Mzee Mustafa Mangunyuka muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa michezo wa Taifa wilayani Namtumbo ambapo aliwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
D92A8301 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mbunge wa Namtumbo Mh. Vita Kawawa muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuwahutubia mamia ya wakazi wa Namtumbo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa mjini Namtumbo.
D92A8357 D92A8345 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia mamia ya wakazi wa Namtumbo katika Uwanja wa Taifa mjini Namtumbo leo.
D92A8357 
Mamia ya Wakazi wa Namtumbo waliohidhuria mkutano wa hadhara ulihutubiwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Uwanja wa Taifa mjini Namtumbo (Picha zote na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment