TANGAZO


Thursday, July 3, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi azindua ujenzi wa Barabara ya Mayamaya hadi Babati

 Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally, funguo ya kuwashia mitambo ya kujengea Barabara, kuashiria kuanza rasmi kwa ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga, Babati kwa kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo, zilizofanyika mapema juzi, Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo, wilayani Kondoa. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Mhe. Zabein Mhita.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati mwenye kilemba) na ujumbe alioambatana nao, wakipatiwa maelezo ya mradi wa Barabara kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni inayojenga barabara hiyo, ya China Railway Seventh Group, wakati
alipotembelea kambi ya kampuni hiyo, iliyopo Kijiji cha Kolo wilayani Kondoa, mapema juzi, Julai Mosi, 2014.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe alioambatana nao, wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga, Babati kwa kiwango cha lami, mapema juzi, wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi huo, iliyofanyika Kijiji cha Kolo, wilayani Kondoa. Wengine pichani ni wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group, inayojenga barabara hiyo, kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).
Wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group, inayojenga Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga, Babati, kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) kwa kiwango cha lami, wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (hayupo pichani), wakati wa sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo, zilizofanyika juzi, Julai Mosi, 2014 kwenye Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kolo, wilayani Kondoa waliojitokeza kwa wingi katika sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga, Babati kwa kiwango cha lami, wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (hayupo pichani). Sherehe hizo, zilifanyika
mapema juzi, Julai Mosi, 2014.
Akina mama wakiwa katika kwenye sherehe za uzinduzi huo juzi.
Mkuu wa Mkoa, Dk. Rehema Nchimbi (watatu kulia), akiwa na baadhi ya viongozi, wakiomba dua wakati uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi
Bonga, Babati kwa kiwango cha lami, kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo, wa barabara, zilizofanyika Kijijini Kolo, wilayani Kondoa mapema juzi, Julai Mosi, 2014. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

No comments:

Post a Comment