TANGAZO


Wednesday, July 2, 2014

Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja Mauzo wa Kampuni ya MM Integrated Steel Mills, Shailendra Singh kuhusu bidhaa za mabati yanayozalishwa na kampuni hiyo, wakati alipotembelea banda hilo mara baada ya kuyafungua Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kulia), akizungumza na Wajumbe Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, wakati walipotembelea banda hilo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wapili kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja Mradi wa  Kampuni ya Pipe Industries, Sebastian Kyoni kuhusu aina mbalimbali za mabomba ya kuvutia maji, wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo, mara baada ya kuyafungua  Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo.
Mwelimishaji wa Veta, Emmanuel Bukuku akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Veta, katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. 
Mahasibu kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) George Kadutu akiwaelimisha wanafunzi wa Shule za Sekondari mbalimbali leo jijini Dar es Salaam juu ya shughuli za Taasisi wakati wa maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara. (Picha na GCU- Wizara ya Fedha)
Mwananchi (kulia) akiwauliza maswali wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania(kushoto)  juu ya huduma mbalimbali za Benki hiyo leo jijini Dar es Salam wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha.
Watumishi wa kutoka Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma (kushoto) wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali  waliotembelea banda la Wizara ya Fedha leo, jijini Dar es Salaam juu ya shughuli za Mfuko huo, wakati wa maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA ), Mzee Boma (wa pili kulia) akisaini Kitabu cha wageni leo jijini Dar es Salaam wakati yeye na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Dkt. Joseph Kihanda (kulia) walipotembelea  Banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa TIA Lilian Mpanj u(kushoto) na Mhasibu wa TIA George Kadutu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt. Joseph Kihanda (kulia), akibadilishana mawazo na Wafanyakazi wa TIA kwenye Banda la Wizara ya Fedha leo wakati alipotembelea maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara. Wengine ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TIA Mzee Boma (wa pili kulia) , Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano Lilian Mpanju(kushoto) na Mhasibu wa TIA, George Kadutu.

No comments:

Post a Comment