Balozi wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam , John
Solombi anasema kuwa balozi huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga
risasi Jumanne usiku na kufariki akiwa anapokea matibabu hospitalini.Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene amethibitisha taarifa hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi wa Libya mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.
Uchunguzi unafanyika kubaini sababu ya kujiua kwa balozi hiyo.
No comments:
Post a Comment