TANGAZO


Monday, June 30, 2014

Matukio mbalimbali ya Maonesho ya Sabasaba Dar leo

Mbunifu wa kifaa cha Elimu ya Mfumo wa Elimu ya Jua na Sayansi ya Anga kutoka Veta, Ernest Daniel, akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda hilo, jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi kama mfano wa sayari zinavyolizunguka jua, wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaa leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mjasiriamali Jonensia John (kulia) wa Kampuni ya Jone Fresh Soap and Culture Fashion, akiwapatia maelezo wananchi waliotembelea kwenye banda na Pride kwenye maonesho hayo leo.
Mmoja wa wasanii aliyevalia kinyago akigawa vipeperushi kwa wananchi waliokuwa wakiingia kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo.
Wananchi wakiangalia bidhaa za maji ya Uhai kwenye banda la Kampuni ya S. S. Bakhesa (Azam) kwenye maonesho hayo.
Maofisa wa Benki ya NMB, Domona Tarimo (wa kwanza kulia) na Shilla Senkoro, wakiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la benki hiyo kwenye maonesho hayo leo.

No comments:

Post a Comment