TANGAZO


Saturday, May 3, 2014

Waziri Mkuu Pinda azindua Wiki ya Elimu Dodoma

Mratibu wa Taifa wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Tehama, Dk. Elia Kibga akimuonesha jambo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea Banda la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Elimu inayofanyika Kitaifa Dodoma. (Picha zote na John Banda)
Katibu wa Chama cha Walimu Dodoma George Palapala akimfafanulia jambo Waziri Mkuu Mzengo Pinda alipotembelea Banda la chama hicho lililopo katika viwanja vya Jamhuri kwa ajili ya maonyesho ya elimu yanayofanyika kwa wiki moja mjini Humo.
Wanafunzi wakiwa katika jukwaa la Uwanja wa Jamhuri  wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa wiki ya Elimu  uliofanyika Dodoma ambapo maonyosho hayo yanafanyikia Kitaifa.
Wanafunzi wakiwa katika jukwaa la Uwanja wa Jamhuri wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa wiki ya Elimu  uliofanyika Dodoma ambapo maonesho hayo yanafanyikia Kitaifa.
 Mwanafunzi Mandela Mazengo (9), mwenye ulemavu wa macho akimuandikia neno kwa kutumia kifaa maalum kinachoandika maandishi yanayoweza kusomwa na wasioona kwa njia ya vidole wakati alipotembelea Banda la shule ya wasioona ya Bwigili Iliyop Chamwino Dodoma, Pinda alifika kuzindua wiki ya elimu iliyoanza Aprl 3,2014 yanayofanyika kitaifa mkoani humo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwauliza baadhi ya wanafunzi waliofika kwenye uzinduzi wa wiki ya elimu uliofanyika katika uwanja wa jamhuri ambao unaofanyika Kitaifa mkoani Dodoma, kama wana uelewa kuhusu neno Big Results now akiwa na maana ya matokeo makubwa sasa kielimu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aakiangalia Tufe lenye mfano wa Ramani ya Dunia ambalo ni maalumu kwa kufundishia wanafunzi wenye ulemavu wa kuona wanaosoma katika shule Iliyopo Bwigili Wilayani Chamwino, alipokuwa akikagua mabanda ya maonesho kwenye uzinduzi wa Wiki ya Elimu inayofanyika Kitaifa Dodoma.

No comments:

Post a Comment