Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza
na ujembe wa watu kutoka Congo hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake
kuwaalika wasanii kutoka Tanzania kushiriki katika sherehe za fiesta nchini
Congo kwa lengo la kudumisha amani na mshikamano katika nchi za maziwa makuu.
Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akifafanua
jambo kwa wajumbe wa maandalizi ya fiesta kutoka Congo walipomtembelea ofisini
kwake, kulia ni mratibu wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bw. Faso Mushigo
Celestin na katikati ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne
Gizenga.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wapili
kushoto akipokea zawadi kutoka kwa wajumbe kutoka Congo waliokuja nchini
kuwaalika wasanii wa Tanzania kushiriki fiesta nchini Congo, kushoto ni
Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiangalia
CD iliyorekodiwa matukio mbalimbali ya fiesta ya mwaka jana ilivyokuwa nchini
Congo. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga. (Picha
zote na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM)
No comments:
Post a Comment