Wanajeshi wawili wa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wamepatikana na hatia ya ubakaji kati wanajeshi 39
walioshitakiwa kwa makosa ya kivita mashariki mwa nchi hiyo.
Wengine waliobaki wamepunguziwa makosa kutoka
makosa ya uhalifu wa kivita lakini wamehukumiwa kwa makosa mengine kama
vile uporaji lakini wengi waliachiwa.Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa kusababisha machafuko katika mji mdogo wa Minova.
Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.
Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanadaiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale wa serikali.
No comments:
Post a Comment