TANGAZO


Sunday, May 25, 2014

Shinawtra aachiliwa huru na Jeshi

Yingluck Shinawtra
Kuna taarifa kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, Yingluck Shinawtra, ameachiliwa huru na viongozi wapya wa jeshi, siku mbili baada ya kuwekwa kizuizini.
Duru ndani ya baraza la kijeshi linaloongoza nchi, zimeliambia BBC, kwamba Bibi Shinawtra, ameambiwa asijishughulishe na siasa, na anahitaji kibali akitaka kutoka nje ya nchi.
Bi Shinawtra alikuwa mmoja kati ya wanasiasa, wasomi na wadadisi, kama mia-moja-na-50, ambao walifungwa baada ya jeshi kunyakua madaraka Alkhamisi.
Wengi bado wako kizuizini.
Maandamano madogo lakini ya hasira, yameendelea kwa siku ya tatu mjini Bangkok, na kuzusha mapigano na baadhi ya watu kukamatwa, lakini hapakuwa na mapambano makali na askari wa usalama.

No comments:

Post a Comment