TANGAZO


Tuesday, May 27, 2014

Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Afrika zafana jijini Dar es Salaam

 

Wanafunzi wakiwa wamebeba bendera mbalimbali za nchi za Afrika na ile ya Umoja wa Afrika wakiwa katika maandamano kuelekea Viwanja vya Karimjee.
Brass band ikiongoza maandamano ya wanadipolomasia wa nchi za Afrika, watumishi wa Serikali ya Tanzania, wanafunzi na wageni wengine waalikwa kwenda Viwanja vya Karimjee kuadhimisha Siku ya Afrika.
Waheshimiwa Mabalozi wakiendelea na maandamano.
Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Afrika.
 Burudani ya ngoma katika Viwanja vya Karimjee kusherehekea Siku ya Afrika
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dk. Mahadhi Juma Maalim (Mb), aliyevaa suti ya rangi ya kijivu akipokea maandamno katika Viwanja vya Karimjee.
Balozi wa Kenya akichangia mada Kilimo na Usalama wa Chakula.
Balozi Sweden nchini Tanzania alipata fursa pia ya kuchangia mada katika maadhimisho hayo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. Yamungu Kayandabila naye akitoa neno wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt Mahadhi Juma Maalim akiwahutubia watu waliohudhuria sherehe za Siku ya Afrika. Naibu Waziri alipongeza kaulimbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni Kilimo na Usalama wa Chakula. Alisema usalama wa Chakula ni changamoto ambayo  lazima nchi za Afrika zichukuwe juhudi za pamoja kukabiliana nayo. (Picha zote kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi)

No comments:

Post a Comment