TANGAZO


Wednesday, May 21, 2014

Serikali ya Denmark na tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), wasaini mkataba wa dola za Kimarekani mil. 6 kwa ajili ya utafiti nchini

Balozi mdogo wa Denmark nchini, Steen Andersen (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda wakilitiana saini mkataba wa dola za Marekani milioni 6  Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kusaidia shughuli za utafiti nchini.
Hapa wakibadilisha hati hizo baada ya kutiliana saini.
Wadau na watafiti wakiwa kwenye hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Balozi mdogo wa Denmark nchini, Steen Andersen (katikati) akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda na Mshauri wa Ufundi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya  Danmark nchini, Lasse Moller.
Balozi mdogo wa Denmark nchini, Steen Andersen (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai wa COSTECH, Dk. Flora Tibazarwa. (Picha na habari kwa hisani ya mwaibale.blogspot.com)

Na Dotto Mwaibale
SERIKALI ya Denmark na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) zimesaini mkataba wa dola za Marekani milioni 6 kwa ajili ya kusaidia shughuli za utafiti nchini.

Mkataba huo, ulitiwa saini na Balozi mdogo wa Denmark nchini, Steen Andersen na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk.Hassan  Mshinda  Dar es Salaam leo na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya utafiti toka mikoa kadhaa na vyuo vikuu ili wajifunze utaratibu huo mpya wakupata fedha hizo.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Mshinda alisema fedha hizo zitasaidia kufanyia utafiti mbalimbali hapa nchini tofauti na hapo nyuma ambapo utafiti huo ulikuwa ukifanywa na watafiti kutoka Denmark na kwa eneo walilotaka.


"Hivi sasa Denmark itakuwa ikitoa fedha hizo kwetu na sisi COSTECH tutakuwa tuzazitoa kwa watafiti watakao shinda zabuni tofauti na zamani ambapo walikuwa wakipewa moja kwa moja" alisema Mshinda.

Alisema hatua hiyo itawasaidia watafiti wa ndani kuweza kufanya kazi zao katika maeneo watakayopenda kuyafanyia utafiti na kutoa wigo mpana wa tafiti kwa maendeleo ya Tanzania.

Balozi mdogo wa Denmark nchini, Steen Andersen alisema Denmark itaendelea kusaidia shughuli za utafiti kwa kutoa fedha kwani nchi mbalimbali duniani zinategemea tafiti katika kutekeleza masuala mbalimbali ya maendeleo.


Nchi ya Denmark kwa miaka mingi imekuwa ikisaidia Tanzania kutoa fedha za kufanyia utafiti mbalimbali.

No comments:

Post a Comment