vifo vyazidi Nigeria
Rais wa Nigeria amelaani mashambulizi yaliyotokea mjini Jos ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne jioni.
Rais Jonathan amesema kuwa waliotekeleza mashambulizi hayo ni watu wenye unyama na wakatili.
Inahofiwa kuwa miili zaidi bado iko chini ya vifusi ya majengo yaliyoharibiwa na milipuko hiyo , ambayo ililenga soko lililokuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na hospitali.Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imetegwa ndani ya gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali.
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameseama hatakomesha juhudi za kuangamiza kabisa ugaidi.
'Mji muhimu'
Mji wa Jos unatazamiwa kuwa mji mkuu wa jimbo la Plateau ambalo liko katika eneo la katikati linalo tenganisha kaskazini iliyo na raia wengi zaidi wa kiislamu, na kusini lililojaa wakristu zaidi.
No comments:
Post a Comment