Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme akizungumza na wafanyakazi wa Shirika hilo, wakati alipokuwa akitoa hotuba yake ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day) katika hafla ya kuwatunuku wafanyakazi bora wa Shirika hilo, Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Rasimali za Shirika, John Lukonge na kulia ni Meneja Rasilimali watu wa TPC, Samuel Kasanga. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa katika hafla ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa Shirika hilo pamoja na kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day), Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la posta wa makao makuu na mkoa wa Dar es salaam waliohudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika wakati wa hafla hiyo, Makao Makuu Posta House jijini hivi karibuni.
Postamasta mkuu na afisa mtendaji mkuu wa shirika la posta ndugu Deos Khamisi Mndeme(waliokaa mstari wa mbele katikati) akizungumza na meneja raslimali watu ndugu Samuel Kasanga

Wafungua champeni wakati wa hafla hiyo Ndugu Hilda Kipara (kushoto) na Ndugu Vailet Mkapa wakiwa tayari kutekeleza wajibu wao.

Na Lucy Ngowi
POSTAMASTA Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme amesema kuwa, amepokea risala ya wafanyakazi hivyo atafanyia kazi masuala yaliyomo kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kudumisha utawala bora.
Mndeme alisema hayo alipokuwa akipokea maandamano ya wafanyakazi wa Makao Makuu na Mkoa wa Dar es Salaam ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani.
Alisema anaamini kuwa uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu ni msingi imara katika kutekeleza kauli mbiu ya Mei Mosi mwaka huu inayosema, ‘ utawala bora utumike kutatua kero za wafanyakazi,’.
“Nawasihi wafanyakazi na viongozi wa ngazi zote tuendeleze ushirikiano na mshikamano katika kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya mwaka huu,” alisema Mndeme.
Awali, Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano (Teuta), Edwin Tibanywana alisema kuwa, wafanyakazi wanafanya kazi katika hali ngumu inayochangiwa na maslahi duni, hivyo imekuwa ni kichocheo kikubwa cha kuwanyima hamasa ya kufanya kazi.
“Mishahara ni duni haiendani na maisha ya binadamu kwa sasa,” alisema na kuongeza kuwa, wakati wafanyakazi wa chini wanataabika wakubwa wanaweka mipango thabiti ya maisha yao.
Alisema kuwa, shirika hilo lina majengo mengi ambayo kuna wapangaji lakini hakuna juhudi binafsi za kukusanya kodi hali inayolirudisha nyuma.
No comments:
Post a Comment