Jaji katika kesi inayomkabili
Oscar Pistorius anasema kuwa mwanariadha huyo lazima aanza kufanyiwa
uchunguzi wa kiakili kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa mwezi mmoja kubaini
hali ya akili yake alipomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Jaji Thokozile Masipa aliamuamuru Pistorius kua
awe anakwenda katika hospitali ya maradhi ya kiakili ya Weskoppies mjini
Pretoria kila siku kuanzia tarehe 26 mwezi Mei.Amri ya jaji inakuja baada ya shahidi mmoja wa upande wa mashitaka kusema kuwa mwanariadha huyo anakumbwa na matatizo ya kuzongwa na mawazo pamoja na kuwa na wasiwasi wakati wote
Bwana Pistorius amekanusha madai ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kusudi
Anasema kwamba kwa bahati mbaya alimpiga risasi kupitia mlango wa choo baada ya kushikwa na wasiwasi akidhani kuwa alikuwa jambazo aliyevamia nyumba yake.
No comments:
Post a Comment