TANGAZO


Saturday, May 24, 2014

Papa azuru Mashariki ya Kati


Msichana katika uwanja wa ndege wa Amman akisubiri Papa Francis kuwasili, huku abeba picha za Papa na Mfalme Abdullah wa Jordan
Akianza ziara ya siku tatu katika Mashariki ya Kati, Papa Francis amesihi kutafutwe suluhu ya amani katika vita vya Syria.
Alisema hayo katika mji mkuu wa Jordan, Amman, katika ziara ambapo piya atafika Ufukwe wa Magharibi na Israil.
Ameongoza sala katika uwanja wa michezo wa taifa wa Jordan mbele ya maelfu ya watu.
Lengo la ziara ya Papa ni kuzidisha ushirikiano na Wakristo wa madhehebu ya Orthodox katika Mashariki ya Kati, na kutoa matumaini kwa Wakristo ambao wanazidi kupungua katika Mashariki ya Kati.
Rabbi na imam wanasafiri na Papa, kusisitiza msimamo wake kuwa Wakristo, Waislamu na Wayahudi wanaweza kuishi pamoja kwa amani.

No comments:

Post a Comment