TANGAZO


Thursday, May 1, 2014

Nigeria yajitetea kuhusu waliotekwa

Wanajeshi wa Nigeria wakiwasaka Boko Haram

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nigeria ameiambia BBC kuwa nikutoitendea haki serikali kwa kuilamu kuwa haikufanya chochote kuwaokoa wasichana wapatao mia mbili waliotekwa.

Waziri Abba Moro amesema Nigeria imefanya kila linalowezekana kuwaokoa wasichana hao lakini inatokana na unyeti wa operesheni yenyewe japo hakufafanua kwa undani unyeti wenyewe.
"Waziri Abba Moro amesema Nigeria imefanya kila linalowezekana kuwaokoa wasichana hao lakini inatokana na unyeti wa operesheni yenyewe japo hakufafanua kwa undani unyeti."
Maoni ya Waziri huyo yakakuja wakati mamia ya wanaigeria hasa wanawake waliamua kuandamana katika mji mkuu wa Abuja wakishinikiza hatua zaidi kuchukuliwa na serikali ili kuwaokoa wasichana hao.
Wasichana hao walitekwa wiki mbili zilizopita wakiwa katika mabweni ya shule iliyopo Kaskazini mashariki na kundi linalosaidikiwa kuwa ni wapigani wa Kiislamu wa Boko Haram

No comments:

Post a Comment