TANGAZO


Saturday, May 24, 2014

Mwenyekiti na Katibu wake, Chadema Mjini Kiomboi wilayani Iramba waachia ngazi wajiunga na CCM

Pichani katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Kata ya Shati, wilayani Iramba, Bw. Ezekiel Makala  akionesha kadi yake na kutangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi ya Kiomboi, wilayani Iramba, mkoani Singida, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba wakishuhudia kwa pamoja.

Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye, katika ziara ya kukagua, kuhimiza na kusukuma mbele miradi ya maendeleo, inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Pichani Kati ni Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Shati, Wilayani Iramba, Bw. Ezekiel Makala  pamoja na Katibu wake Bw. Joseph Kingu wakitangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi ya Kiomboi, wilayani Iramba, mkoani Singida, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba wakishuhudia kwa pamoja.
Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Shati,Wilayani Iramba, Bw. Ezekiel Makala  pamoja na Katibu wake Bw. Joseph Kingu sambamba na wanachama wengine kutoka chama hicho cha CHADEMA, Bw. Ayoub Gofrey kutoka kata ya Makunde, Julius Kizanda kata ya Mtekente na Ally Saleh kata ya Kisila wakila kiapo cha utii mara baada ya kutangaza rasmia kuachia ngazi nafasi zao na kuhamia chama cha CCM, kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika leo jioni kwenye stendi ya mabasi ya Kiomboi, wilayani Iramba mkoani Singida.

Viongozi hao wa CHADEMA walikiri wazi kwenye mkutano wa hadhara kuwa chama cha CCM, ndicho chama bora na kitaendelea kutokuwa na mpinzani siku hadi siku, kwa sababu kinaonesha nia ya dhati ya kuwa karibu na wananchi ikiwemo na kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo yao.

Katibu wa NEC, Itikadi Siasa na Uenezi, Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Shelui mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana,huku Katibu wa NEC,Itikadi Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akisikiliza, hayo yamefanyika leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa sokoni mjini Shelui wilayani Iramba mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopata umeme katika Wilaya ya Iramba, jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shelui mkoani Singida.
Wananchi wa Kiomboi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara jioni leo, katika stendi ya mabasi ya Kiomboi, Wilayani Iramba mkoani Singida.
Wananchi wa Kiomboi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara jioni ya leo, katika stendi ya mabasi ya Kiomboi, Wilayani Iramba mkoani Singida.
Katibu wa NEC, Itikadi Siasa na Uenezi, Nape Nnauye akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika stendi ya mabasi ya Kiomboi, wilayani Iramba mkoani Singida.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika stendi ya mabasi ya Kiomboi, Wilayani Iramba mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment