TANGAZO


Monday, May 26, 2014

Marehemu Amina Ngaluma azikwa jijini Dar es Salaam

Waombolezaji wakiwasili msibani.


MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Amina Ngaluma, amezikwa leo mchana katika Makaburi ya Kitunda Machimbo, jijini Dar es Salaam, kuashiria kuwa sura au sauti ya mkali huyo haitosikika wala kuonekana tena.

Ngaluma aliyefariki nchini Thailand, mwili wake uliletwa jana usiku, ambapo wadau na mashabiki wa muziki wa dansi Tanzania, walipata fursa ya kushiriki katika mazishi yake.

Tofauti na wakati wa mapokezi ambapo wanaamuziki walishindwa kuhudhuria, jana katika mazishi hali ilikuwa nzuri kwa wadau wengi kujitokeza.
Waombolezaji (akinamama), wakiwa katika msiba huo.

Waombolezaji wakisubiri taratibu za mazishi.
Kutoka kushoto, Mzee Kitime, Rashid Sumuni na Ali Choki, wakipata chakula msibani hapo.
AustraliaWaombolezaji wakitoka Msikitini tayari kwa kwenda kwenye maziko.
Mwili wa Amina Ngaluma
Jenenza lenye mwili wa marehemu Amina Ngaluma, likiingizwa kwenye Makaburi tayari kwa ajili ya mazishi leo.
Amina Ngaluma Akiwekwa KaburiniMume wa marehemu Amina Ngaluma akisoma dua kwa mkewe.
Amina Ngaluma Afariki DuniaMwili wa marehemu Amina Ngaluma ukishushwa tayari kuingia kaburini kwa maziko, Machimbo Mnarani.
Kaburini la Marehemu Amina NgalumaKaburi la marehemu Amina Ngaluma aliyezikwa leo maeneo ya Machimbo, Mnarani. (Picha zote kwa hisani ya Global Publishers)

No comments:

Post a Comment