TANGAZO


Sunday, May 11, 2014

Mapigano yazuka upya Sudan Kusini


Salva KIir (kushoto) na Riek Machar wakipeana mkataba waliotia saini Addis Ababa

Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wamelaumiana kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano - masaa tu baada ya makubaliano kufikiwa.
Msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, alisema wapiganaji wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu leo alfajiri.
Wapiganaji wamewashutumu wanajeshi wa serikali kuwa waliwashambulia katika sehemu kadha katika majimbo ya Upper Nile na Unity.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni moja kuhama makwao.

No comments:

Post a Comment