Watafiti wa Marekani wamebaini miili ya watoto hao hutoa viini vya kinga ambavyo hushambulia wadudu wanaosababisha Malaria.
Kwa kumdunga mtu sindano yenye viini hivyo vyo mtu anaweza kukingwa na ugonjwa huo .Prof Jake Kurtis, mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa afya wa kimataifa katika hospitali ya kisiwa cha Rhode katika chuo kikuu cha tiba cha Brown , alisema : "Nadhani kuna ushahidi wa kuaminika kwamba hii inaashiria upattikanaji wa chanjo ''
" Hata hivyo wadudu wa malaria ni vigumu kuwashambulia'' . Kwa kweli ni maadui wakubwa ." aliongeza Kurtis. Utafiti huo ulianza kwa kundi la watoto wa shule 1000 nchini Tanzania , ambao sampuli za damu yao zilichunguzwa mara kwa mara katika miaka ya mwanzo ya maisha yao .
Asilimia 6 ya watoto ya watoto hawa waliweza kuwa na kinga asilia kwa malaria, licha ya kuishi katika eneo ambako ugonjwa huo umekithiri.
No comments:
Post a Comment