TANGAZO


Friday, May 23, 2014

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana aendelea na ziara yake ya siku 4 mkoani Singida

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndugu Abdulrahman Kinana, akishiriki ujenzi wa Ofisi za chama hicho, Kata ya Ighombwe, ambapo aliwahimiza viongozi wa CCM kujenga ofisi zenye uwezo wa kutoa msaada wa kijamii, ikiwa ni pamoja na Elimu za ujasiriamali. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio)

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Ighombwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia.
 Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kata ya Ighombwe na kuwataka kudumisha moyo wa mshikamano katika kuleta maendeleo ya pamoja.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Ighombwe, wakila kiapo baada ya baadhi yao, kujiunga na chama hicho, cha CCM katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana (haoenekani pichani), akizungumza na wananchi baada ya kushiriki ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Sepuka, wilayani Ikungi.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Sepuka, wilayani Ikungi, Jimbo la Singida Magharibi na kuwataka kuungana katika kushiriki kuleta maendeleo, hasa yale yanayohusu jamii kama kujenga shule, maabara na zahanati.
Wananchi wakiwa katika mkutano huo, wakinyanyua mikono kumunga mkono Katibu Mkuu Kinana.
Mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM, ukiendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Sepuka, wilayani Ikungi, Singida Magharibi.
 Katibu MKuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana (haonekani vizuri pichani), akizindua shina la Vijana wa Bodaboda katika Kata ya Puma, wilayani Ikungi, mkoani Tabora.
Katibu MKuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akizindua shina la Kina mama wa UWT, ambao hujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali, ikiwemo, ushonaji wakiwa katika kikundi cha Ebeneza, Puma, wilayani Ikungi, mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kuvuna viazi vitamu pamoja na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai kwenye shamba la mkulima Bernardo Razalo.

No comments:

Post a Comment