Mamlaka nchini Libya imesema kuwa imeshindwa kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaotaka kuingia Ulaya kwa kutumia mlango wa nyuma.
Inadaiwa kuwa zaidi ya raia laki tatu wamo nchini Libya wakitaka kuvuka bahari ya Mediterenean.Wale wanaokamatwa wakitaka kuanza safari hiyo huwekwa katika jela ndogo ambazo zimejengwa katika pwani ya bahari hiyo.
Mwandishi wa BBC katika mji wa bandari ya Misrata amesema kuwa Libya sasa ndio mlango wa raia wa afrika kuingilia Ulaya.
Muungano wa Ulaya umeonya kuwa mwaka 2014 utakuwa na wahamiaji wengi watakaowasili katika fukwe za mataifa ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment