TANGAZO


Tuesday, May 27, 2014

Guinea yasaini mkataba mkubwa wa madini


Mkataba huu ni mkubwa zaidi kuwahi kutiwa saini na kampuni ya Rio Tinto
Serikali ya Guinea imesaini mkataba mkubwa zaidi wa uchumbaji madini na makampuni ya Rio Tinto, Chinalco ya Uchina na shirika la kimataifa la fedha.
Mkataba huo unakisiwa kuwa wa zaidi ya dola bilioni 20 ukiwa mkubwa zaidi wa uchimbaji madini barani Afrika.
Uchimbaji wa mgodi wa Simandou unatarajiwa kutoa kiwango kikubwa zaidi ya madini ya chuma na hivyo kuinua sekta ya viwanda na uchumi wa nchi kwa jumla.
Inakisiwa kuwa Simandou ndio mgodi ulio na viwango vya juu zaidi vya chuma duniani. Lakini kuchimba chuma hiyo kutahitaji uwekezaji mkubwa zaidi na sio tu katika uchimbaji wake bali pia usafirishaji wake.
Kikundi cha waekezaji kinachoongozwa na Rio Tinto kimekubali kujenga mgodi huo pamoja na reli ya urefu wa kilomita 650 hadi ufuo wa bahari ya Atlantic.
Na sio hiyo tu, bali pia bandari kubwa katika ufuo huo.
Waekezaji wa Nje wataruhusiwa kuchangia katika ujenzi huo wa dola bilioni ishirini kwa makubaliano kuwa watafaidi kutokana na biashara ya reli hiyo na bandari.
Serikali ya Guinea inaamini kuwa mradi huo mpya utaimarisha uchumi wa nchi kwa asili mia mia moja na kutoa zaidi ya nafasi 45000 mpya za ajira.

No comments:

Post a Comment