Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngondo (kulia) akiwa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la Ufa leo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala akisisitiza umuhimu wa mkutano wa wadau wa TEHAMA katika nchi za Bonde la Ufa na msatakabali wa vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (katikati) akisalimiana na baadhi ya
washiriki mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau Teknolojia ya habari na
mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es
salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-
Maelezo
Serikali imejenga
mazingira mazuri kwa wawekezaji ili kuvutia makampuni mbalimbali kuwekeza
kwenye sekta ya mawasiliano nchini.
Kauli hiyo imemtolewa
na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa alipokuwa
akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)
kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
“Nawasihi wajasiriamali
katika mambo ya TEHAMA ndani ya nchi washirikiane na wenzao wa nje ya nchi ili waweze
kujijengea uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa aliwasihi
washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza
katika TEHAMA ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano
katika maeneo yote nchini hadi vijijini.
Aidha, Prof. Mbarawa
alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya TEHAMA ni pamoja na ukosefu wa
nishati ya umeme vijijini, kumudu gharama za uendeshaji, ukosefu wa vifaa vya
sekta hiyo na usalama wa taarifa mbalimbali katika mitandao.
Kwa upande wake Waziri
wa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa Bunge kutoka Burundi, Tharcisse
Nkezabahizi alisema kuwa TEHAMA ni moja ya Nyanja muhimu inayotumiwa katika
nchi yake ikiwemo elimu na huduma za afya ambapo ni muhimu kwa nchi za bonde la
ufa kutumia teknolojia hiyo ili kukuza uchumi wan chi husika.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala alisema
kuwa mkutano huo umekuja wakati mwafaka ambapo nchi nyingi zinatumia fursa iliyopo
ili vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.
Tanzania mpaka sasa
imekuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika kutekeleza hatua ya kuhama
kutoka mfumo wa analogia kwenda dijiti mbapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka
huu takribani mikoa yote itakuwa imezima mitambo ya analojia kwenda dijiti.







No comments:
Post a Comment