TANGAZO


Tuesday, April 29, 2014

Mwandishi wa Voice of America amtembelea Waziri wa Habari Zanzibar, Mhe. Said Ali Mbarouk

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk, akizungumza na Mwandishi wa habari wa  Voice of American Dkt. Shaka Ssali., alipofika Ofisini kweke kwa mazungumzo. 
Mwandishi wa habari mkongwe Dkt. Shaka Ssali, akizungumza na Waziri wa habari alipofika Ofisini kwake Kikwajuni kwa mazungumzo juu ya maendeleo ya Afrika. katika sekta ya habari.
Dkt. Shaka Ssali akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumzia habari za Bara la Afrika, alipokutana na Waziri wa habari na Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi wa wizara ya habari Kikwajuni.  
Viongozi wa Wizara ya Habari Zanzibar wa kwanza Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Bi Bihindi Hamad, Mkurugenzi Mipango wa Wizara hiyo Mhe. Joseph Kilangi na Mkuu wa Taaluma wa Chuo cha Habari Zanzibar Rashid Omar wakifuatilia mkutano huo.

Ofisa wa Ubalozi wa Marekani Tanzania Bwa. David Feldmann, akizungumza na kumtambulisha Dkt. Shaka Ssali kwa Waziri na Waandishi wa Habari wa Zanzibar, katika ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Waandishi wakipata habari katika mkutano huo.

Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Kikwajuni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment