TANGAZO


Wednesday, April 30, 2014

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo akutana na waandishi wa habari


*Wizara yamaliza kazi ya kuipitia Katiba ya Simba

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania Ndg. Leornad Thadeo, akifafanua na kutowa kwa waandishi wa kuhusiana na Rasiomu ya Katiba ya Timu ya mpira wa miguu ya Simba baada waandishi kutaka ufafanuzi juu ya Katiba ya Uchaguzi Klabu ya Simba. 















Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania Ndg. Leornad Thadeo,akiwaonesha waandishi habari Rasimu ya Katiba ya Timu ya Simba, baada ya wandishi kutaka ya Uchaguzi Mkuu wa Timu ya Simba, unaotaraji kufanyika wakati wowote.(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)


Na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)
30TH April, 2014
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali za waandishi leo jijini Dar es Salaam.

Akijibu moja ya hoja iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika upatikanaji wa Katiba ya Club ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji wa Katiba umemelizika na kuonekana kuwa na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha katiba hiyo.

“Mchakato wa upitiaji wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini kumekuwepo na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha Katiba hiyo” amesema Bw. Thadeo.

Akifafanua zaidi Bw. Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande wa kisheria ambapo mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana tofauti na Katiba ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya marekebisho hayo mapema na kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya kuidhinishwa.

Aidha Bw. Thadeo amewataka waandishi wa habari pamoja na wanachama wa Club ya Simba kuwa na subira ili waweze kupata Katiba itakayokidhi malengo ya Club yao kwani mchakato wa upitiaji wa Katiba ulihitaji umakini.   

No comments:

Post a Comment