Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, akitoa hoja ya kutengua Kanunia za bunge hilo kwa ajili ya kutoa muda zaidi katika hotuba za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa kuaghirishwa bunge hilo leo hadi Agosti 5, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifuatilia michango iliyokuwa ikitolewa na wajumbe mbalimbali wa bunge hilo, ukumbini humo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Modestus Kilufi na Magdalena Rwebangira, wakiangalia jambo kwenye kitabu wakati wa kikao cha bunge hilo, cha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za bunge hilo, akijadili jambo na mjumbe mwenzake ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Issac Cheyo, akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Jina Hassan Silima akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Jina Hassan Silima akichangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Kingunge Ngomable Mwiru na Eng. Stelle Manyanya wakifuatilia michango ya wajumbe, wakati wa kikao cha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba, Januari Makamba na Angela Kairuki wakijadili jambo wakati wa kikao cha kuchangia vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Saningo Ole Telele, wakizungumza jambo wakati wa kikao hicho, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Augustin Mrema (kushoto), akimsikiliza mjumbe mwenzake Mohamed Aboud Mohamed, wakati alipokuwa akimsomea jambo, wakati wa kikao cha Bunge hilo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zainab Vulu (kushoto) na Dk. Mary Mwanjelwa wakizungumza jambo nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, akizungumza na wajumbe wa Bunge hilo, wakati alipokuwa akiliaghirisha hadi Agosti 5, mwaka huu.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na wajumbe wa bunge hilo, wakati wa kuaghirishwa kwa bunge hilo mpaka Agosti 5, mwaka huu, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na wajumbe wa bunge hilo, wakati wa kuaghirishwa kwa bunge hilo mpaka Agosti 5, mwaka huu, mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment