Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakielekea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha kuapishwa, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakiwa mbele ya lango la kuingilia ndani ya ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha kuapishwa, mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, akishauriana jambo na Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad, kabla ya kuanza kikao cha kuwaapisha wajumbe wa bunge hilo, katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, akieleza jambo kwa wajumbe, wakati wa kuanza kwa kikao cha kuwaapisha wajumbe wa bunge hilo, katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Rashid Ali Omar, akila kiapo cha uaminifu na utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitumikia kwa wajibu na kazi ya bunge hilo zilizoko mbele yake, wakati wajumbe wa bunge hilo, walipokuwa wakiapa ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo kabla ya Jumatatu kuanza kazi rasmi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuwasilisha rasmi Rasimu ya Pili ya Katiba bungeni humo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Maria Sarungi, akila kiapo cha kuwa mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano, wakati wa kuapishwa kwa ajili ya bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Vita Kawawa akiapa kuwa mtiifu na kuitumikia kwa uaminifu Jamhuri ya Muungano katika kazi zake za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Panya Ali Abdalla, akiapa kuwa mtiifu na kuitumikia kwa uaminifu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zake za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho (kushoto) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakifuatilia jambo, wakati wajumbe walipokuwa wakila viapo vya utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zao za kulitumikia bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo, Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho wakizungumza jambo, wakati wajumbe walipokuwa wakila viapo vya utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zao za kulitumikia bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mahamoud Thaabit Kombo, akila kiapo hicho, bungeni humo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Idd Azzan, akiapa wakati wa kikao hicho cha kuwaapisha, bungeni mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Margreth Sitta, akiapa kuwa mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano, wakati wa kuapishwa kwa ajili ya kuwa mbunge wa bunge hilo, mjini Dodoma
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Maua Abeid Daftari, akiapa kuwa mtiifu na kuitumikia kwa uaminifu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zake za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mbaraka Igangula, akiapa kuwa mtiifu na kuitumikia kwa uaminifu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kazi zake za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mbwana Kibanda, akila kiapo cha uaminifu na utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitumikia kwa wajibu na kazi iliyo mbele yake.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kutoka taasisi za Dini, Sheikh Mussa Kundecha, akiapa kuwa mjumbe wa bunge hilo, ndani ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa bunge hilo, Maalum la Katiba, Vicky Kamata, akila kiapo cha utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulitumikia bunge hilo kwa uaminifu.
Mjumbe wa bunge hilo, Maalum la Katiba, Ester Bulaya, akila kiapo cha utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulitumikia bunge hilo kwa uaminifu.
Wajumbe wa bunge hilo, wakifuatilia jambo wakati wajumbe wenzao wakila kiapo hicho cha utiifu.
Mjumbe wa bunge hilo, Maalum la Katiba, Lucy Mayenga, akila kiapo cha utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulitumikia bunge hilo kwa uaminifu.
Mjumbe wa bunge hilo, Maalum la Katiba, Zainab Kawawa, akila kiapo cha utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulitumikia bunge hilo kwa uaminifu.
Mjumbe wa bunge hilo Maalum la Katiba, Magreth Mbene, akila kiapo cha utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulitumikia bunge hilo kwa uaminifu.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, akitoa maelekezo kwa wajumbe wa bunge hilo, mara baada ya kumaliza kuwaapisha wajumbe na kuaghirisha kikao cha bunge hilo hadi Jumatatu saa 3 asubuhi.
No comments:
Post a Comment