Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akiongoza mamia ya wananchi pamoja na viongozi wa Serikali, Siasa na Dini wa Mji wa Dodoma
na Vitongoji vyake katika kuuaga mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, marehemu
John Tuppa, mjini Dodoma jana. Nyuma
yake Balozi Seif alifuatiwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Mke wa
Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Anna Makinda.
Mwili
wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Gariel Tuppa aliyefariki Dunia
Juzi Tarehe 26/3/2014, ukiingizwa ndani ya Bunstani ya Nyerere Square
kati kati ya Vitongoji wa Mji wa Dodoma kwa ajili ya Ibada Maalum ya
Kuuaga jana.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Pili kutoka Kulia akiwaongoza Mamia ya
wakaazi wa Mji wa Dodoma katika kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa
Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Gariel Tuppa ndani ya Viunga vya
Nyerere Square Mjini Dodoma. Kulia
ya Balozi Seif ni Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda, Mke wa Waziri Mkuu Mama
Tunu Pinda na Spika wa Bunge la Muungano Mh. Anna Makinda na kushoto
yake Balozi Seif, ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi.
Mke wa
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, marehemu John Gariel Tuppa Mama Tupa
Gabriel (wa pili kulia) pamoja na wana familia ya marehemu wakiwa
kwenye Misa ya kuuaga mwili wa marehemu mumewe, ndani ya Bustani ya
Nyerere Squre, Mjini Dodoma jana.
Wana
Kwaya ya Mtakatifu Sifiria chini ya muongozaji wao, Francis Patrick
wakiendelea na nyimbo za Ibada katika Misa ya kuuaga mwili wa Mkuu wa
Mkoa wa Mara, marehemu John Gariel Tuppa. (Picha zote na Hassan Issa OMPR)
Na Othman Khamis, OMPR
Mamia
ya wananchi na Wakaazi wa Mji wa Dodoma na vitongoji vyake jana wameuaga
rasmi mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tuppa
aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime
Mkoani Mara.
Marehemu
John Gariel Tuppa alilazimika kupatiwa huduma za matibabu baada ya
kuugua ghafla ugonjwa wa Shindikizo la Damu { Blood Pressure } akiwa
katika Vikao vya kazi Wilayani Tarime.
Misa
ya kumuombea Mkuu huyo wa Mkoa wa Mara iliyoongozwa na Makamu Askofu wa
Kanisa Katoliki la Mkoa wa Dodoma Father Chesco Msaga ilifanyika katika
Uwanja wa Nyerere Suare kati kati ya Vitongoji vya Makao Makuu ya
Serikali Mjini Dodoma.
Wakiwa
katika hali ya majozi mamia ya wananchi hao wakiongozwa na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri Mkuu wa Serikali
ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda, Mawaziri wa Serikali zote
mbili, Viongozi wa Dini tofauti wakiwemo pia wawakilishi wa mashirika na
Taasisi za Kimataifa walipata fursa ya kuuaga mwili wa Maheremu John
Gabriel Tuppa.
Wakiwasilisha
salamu mbali mbali wawakilishi wa Serikali, Viongozi wa Dini na Taasisi
tofauti za Kijamii walimueleza Marehemu John Gabriel Tuppa kwamba ni
Kiongozi wa mfano atakayekumbukwa miaka kadhaa ijayo kutokana na mchango
wake hasa katika masuala ya Kijamii.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. William Lukuvi alisema miaka 20 ya
Utumishi wa Marehemu John Gariel Tuppa ndani ya Manispaa ya Makao Makuu
Mjini Dodoma (CDA) utaendelea kukumbukwa na wananchi walio
wengi Mkoani humo.
No comments:
Post a Comment