Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga(mbele aliyesimama), akiongea na Maofisa Habari na Mawasiliano kuhusu ushirikiano wa Serikali na Vyombo vya Habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini. Wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Habari na Mawasiliano jana, Mkoani Tanga.
Na Assah Mwambene, Tanga
BARAZA la Habari Tanzania limesema
kuna haja ya kujenga miundombinu itakayoboresha ushirikiano kati ya Maafisa
Habari na Vyombo vya Habari ili kuboresha utendaji kazi katika tasnia ya
habari.
Akizungumza katika kikao kazi cha Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini kinachoendelea mjini Tanga, Katibu Mtendaji wa MCT, Bw. Kajubi Mukajanga amesema
ili sekta ya habari iweze kuboreka ni lazima kuwe na ushirikiano wa kutosha
kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari.
Alisema kimsingi vyombo vya habari
vinatakiwa kufanya kazi kwa pomoja kutokana na ukweli kwamba kila upande
unamhitaji mwenzake ili kutimiza
majukumu yake.
“kimsingi tunahukumiwa kufanya kazi
kwa pamoja” alisema Bwana Kajubi, akinukuu sehemu ya Hotuba aliyotoa Mhe. Rais
Jakaya mrisho Kikwete katika moja ya mikutano ya “open Government uliofanyika
London Uingereza.
Akizungumza kuhusu fikra mgando
katika Vyombo vya Habari, alisema kumekuwa na tatizo la baadhi ya wanahabari
kugeuka kuwa wanaharakati na kuvaa fikra ya kupambana na serikali kama
wanavyofanya wanaharakati.
unaowaelekeza wadhani kuwa
wanahabari wako katika mapambano na serikali.
“Kama habari nzuri za serikali
haziuzi mbona Timu ya Taifa au Mwakilishi wa Taifa kwenye mashindano ya
Kimataifa akishinda watu hupenda kusoma” Alisema Bwana Kajubi.
Alisema kwa maoni yake kushikilia kuandika
matatizo tu kuhusu nchi yetu sio kuisaidia nchi na hakujengi moyo wa wananchi
kujiamini na uzalendo.
Bw. Kajubi alikuwa akitoa mada
kuhusu Ushirikiano wa serikali na Vyombo vya habari katika kuimarisha
Mawasiliano Serikalini katika kikao kazi za Maafisa Habari na Mawasiliano.
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mkutano wa Maafisa Habari na
Mawasiliano unawahusisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Wizara, Idara
zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Serikali za Mitaa, Mikoa na mashirika ya
umma wapatao 130 kutoka nchi nzima.


No comments:
Post a Comment