Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu, Dk. William Mgimwa, wakati wa hafla ya kuuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa wakati wa hafla ya kuuaga mwili huo zilizofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo, kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dk. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Dk. Mgimwa, zilizofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu, Dk. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuuaga na kutoa heshima za mwisho, zilizofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo mchana. Mwili huo, umesafirishwa leo kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.
Mawaziri wakilibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Dk. William Mgimwa wakati likipakiwa kwenye gari tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.
Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.
Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, heshima za mwisho.
Baadhi ya Mawaziriki wakiwa katika foleni kuelekea kutoa heshima zao za mwiho.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika shughuli hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo.
Baadhi ya Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
No comments:
Post a Comment