Mtawala wa zamani wa kijeshi nchini Pakistan, Pervez Musharraf
amelazwa hospitali kwa kile kinachoshukiwa kuwa ni matatizo ya moyo, akiwa
njiani kuelekea mahakamani ambako anakabiliwa na mashitaka ya uhaini.
Maafisa nchini Pakistan, wameiambia mahakama kuwa Musharraf mwenye umri wa
miaka 70, alihamishiwa katika hospitali ya kijeshi ya magonjwa ya moyo huko
Rawalpindi.Hii ni mara ya tatu kwa rais huyo wa zamani wa Pakistan kushindwa kufika mahakamani kufuatia matukio mawili yaliyopita kuhusishwa na wasiwasi kutokana na hali ya usalama.
Mashitaka ya uhaini yanahusishwa na uamuzi wake wa mwaka 2007, kusitisha katiba na kutangaza hali ya hatari.
Bwana Musharraf amekana mashitaka hayo na anasema tuhuma zote dhidi yake zinatokana na msukumo wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment