Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu akifafanua jambo wakati akifungua kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya mtandao ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali wa mtandao, kongamano hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya mtandao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada wa kwanza katika kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya mtandao Bw. Said Kalunde akitoa mada iliyohusu uhalifu wa mtandao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini
kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya
mtandao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo)
SERIKALI yaendelea kushirikisha wadau mbalimbali wa mitandao
ili kuweza kupata sheria itakayosimamia matumizi salama ya mitandao hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano la siku mbili mapema
hii leo jijini Dar es Salaam mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu alisema kuwa serikali
inashirikiana na wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa lengo la kupata
maoni yao.
“Kongamano hili linakutanisha wadau muhimu ambao maoni yao
yataweza kufanikisha kupatikana kwa sheria ya mtandao ambayo itakuwa ndiyo
suluhisho la uhalifu wa mtandao ambao unaonekana kushamiri sana hapa nchini na
duniani kwa ujumla,” alisema Profesa Makungu.
Aidha Profesa Makungu aliongeza kuwa katika kupambana na
uhalifu wa mtandao Tanzania imeandaa miswada mitatu ya sheria ya usalama wa
mtandao ambayo pia inatumika katika
Shirikisho la Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC).
“Sheria hizo ni sheria ya mtandao, sheria ya usalama wa
taarifa na sheria ya biashara mtandao kwa kufanya hivi tuko sambamba na Jumuiya
ya afrika Mashariki, Shirikisho la Maendeleo Kusini mwa Afrika na Umoja wa
Afrika ambao wote wana lengo moja la kupambana na uhalifu wa mtandao,”
aliongeza Profesa Makungu.
Naye Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia Dkt. Ally Simba
alisema kuwa kama hakuna sheria ya
mtandao ni rahisi uhalifu wa mtandao kupunguza wawekezaji kwani usalama wa fedha unakuwa ni mdogo.
Serikali inaendelea
kukusanya maoni ya wadau
mbalimbali kuhusu sheria ya mtandao kwani mchakato wa kupata sheria uko katika
hatua za mwisho na ambapo mwakani katika
miezi ya mwanzoni sheria hii itakuwa tayari.
No comments:
Post a Comment