TANGAZO


Friday, October 18, 2013

Shehena ya meno ya tembo yanaswa Uganda

 

Maafisa nchini Uganda wamekamata shehena meno ya tembo yenye uzito wa tani mbili, ambacho ni kiwango kikubwa kukamatwa kwa miaka mingi iliyopita.
 
Chama cha Wanyama Pori nchini Uganda kimesema meno yapatayo 832 yenye thamani ya dola milioni 6.7 yamekamatwa.
 
Wataalamu wanasema baadhi ya meno hayo yanaaminika yametokana na tembo waliouawa na majangili nje ya nchi ya Uganda.
Kuna mahitaji ya meno ya tembo kutoka barani Afrika kwenda nchi Asisa kwa ajali ya kutengeneza mapambo.
Meno hayo ya tembo yalikuwa yakielekea kwenda katika bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Baadhi ya meno hayo yalikuwa yamekatwa vipande vipande na kufunikwa chupa za plastiki kwenye kreti na kubandikwa maandishi kwamba na bidhaa zinazokwenda kuchakatwa.
Chama hicho cha Wanyama pori kimemwambia mwandishi wa habari wa BBC Catherine Byaruhanga kuwa Uganda imeanza kutumika na majangili kama njia ya kupitisha bidhaa za wanyapori kutoka nchi za Sudan Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

Post a Comment