TANGAZO


Saturday, October 26, 2013

Mama wa mapacha watatu aomba msaada wa kuwatunza watioto wake

 
Watoto Hussen, Hassan na Hasanati waliozaliwa mapacha watatu ndivyo wanavyoonekana wakiwa wamebakiza
siku chache kutimiza mwaka tangu wazaliwe. (Picha zote na John Banda)
Rehema Khamis akiwa na watoto wake mapacha watatu na dada yao ambapo hata hivyo kaka yao hakuwe mwenye
umri wa miaka 13, mama huyo anahitaji msaada ili aweze kuwatunza kuwalea.
Rehema Khamis(30) akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha watatu huku wengine wakisubirishwa mpaka wa kwanza amalize kulishwa na mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.
Rehema Khamis (30)akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha watatu huku wengine wakisubirishwa mpaka wa kwanza amalize kulishwa na mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.
 
Na John Banda, Dodoma
MWANAMKE wa mwanajeshi anaomba msaada kwa wasamaria wema ili aweze kuwahudumia watoto wake watatu aliojifungua kwa chakula, mavazi na elimu kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili pamoja na familia yake, kiasi cha kushindwa kupata hata lishe ya kuwapa mapacha hao watatu, kinyume na matarajio yake.

Mwanamke huyo, Rehema Khamis (30), mkazi wa Mkalama, Kata ya Makulu, Manispaa ya Dodoma, ameomba msaada huo baada ya kuona tokea alipojifungua watoto hao, watatu imefika wakati hata kushindwa kuwapatia hata uji wenye lishe huku mshahara wa mumewe huyo ukiishia kwenye madeni anayodaiwa na watu.

Rehema alisema kuwa tokea alijifungua watoto hao, wa kiume wawili na wa kike mmoja, ambao ni Hassan, Hussein na Hasanati katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, ambapo sasa wanakaribia kuwa na umri wa mwaka mmoja, amekuwa akikabiliana na matatizo mengi hadi kulazimika kuwaachisha kunyonya wakiwa na miezi 7 kutokana na kukosekana maziwa ya kutosha.

Alisema kuwa hakutarajia kupata watoto watatu kwa mpigo kutokana na kuwa tayari alishakuwa na wengine wawili, hivyo alijua akipata mmoja angepumzika kuzaa ili ajipe nafasi ya kuwalea, hivyo kutokana na watoto hao kuhitaji chakula, mavazi na hata elimu wawapo wakubwa.

‘’Watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakifika kuwaona watoto wangu hawa lakini ni kama uwanja wa maonyesho tu kwani hakuna hata mtu mmoja aliyekuja kutuona na kasha kutusaidia chochote, watu wanafika kutuona na kisha kuondoka bila kuleta msaada wowote, hivyo ninawaomba wenye uwezo na moyo waweze kutusaidia chochote ili watoto hawa waweze kupata malezi bora", alisema Rehema.

Nae Baba wa watoto hao Abubakari Ally Hamad Mwanajeshi wa ajira mpya katika jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] kikosi cha 673 Msalato Dodoma alisema mahitaji yamekuwa hayatoshelezi kutokana na mshara anaopata kuishia kwenye madeni ambayo amekuwa akikopa kwa wanajeshi wenzake.

Alisema pesa hata madeni hayo ambayo amekuwa akikopa hayatoshelezi mahitaji ya watoto hao ambao hata hivyo hahitaji kuongeza wengine, hata hivyo aliwataka watu mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali kumsaidia kutokana na watakavyojaliwa na mwenyezi mungu ili aweze kuwa tunza watoto wake.

Kwa upande wake Ofisa mtendaji wa kijiji cha makulu Namsfu Mihungo alisema wao kama serekali wanajitahidi kufikisha ujumbe kwa watu kuhusu familia hiyo kuhitaji msaada na kufika kuwaona lakini hawakujua kama hakuna msaada unaotolewa, hivyo watajipanga kuona nini watafanya ili kuisadia familia hiyo kwa kadili watakavyoweza.

No comments:

Post a Comment