TANGAZO


Saturday, October 26, 2013

Ethiopia yapata umeme kutokana na upepo

ya kuzalisha umeme kutokana na upepo

Eneo kubwa kabisa Afrika, kusini ya Sahara, kutengwa kwa ajili tu ya mitambo ya kuzalisha umeme kutokana na upepo, limefunguliwa rasmi nchini Ethiopia.
 
Mradi huo wa Ashegoda karibu na mji wa Mekelle, kaskazini mwa Ethiopia, umejengwa na kampuni ya Ufaransa ya Vergnet SA na Ufaransa ndiyo imetoa nyingi ya dola 290 milioni kugharimia mradi huo.
Serikali ya Ethiopia ililipa 9% ya gharama.
Mradi huo wa kuzalisha umeme kutoka nguvu za upepo utaisaidia Ethiopia siku za ukame ambapo mabwawa hayataweza kutoa nishati nyingi.

No comments:

Post a Comment