Taarifa kutoka nchini Libya zinasema kuwa Saif al-Islam Gaddafi -- mwanawe marehemu Kanali Muamar Gadaffi, hataruhusiwa kusafiri hadi mjini Tripoli kuhudhuria kikao cha kwanza cha maandalizi ya kesi yake kilichotarajiwa kuanza baadaye leo.
Seif alistahili kufika mahakamani kwa kesi dhidi yake pamoja na aliyekuwa mkuu wa ujasusi Abdullah al-Senoussi.
Afisaa,mmoja anayesimamia kuzuiliwa kwake mjini Zintan, ameambia BBC kuwa hali ya usalama sio nzuri kuweza kumhamisha Seif hadi Tripoli.Kikao hicho kinatumiwa kuwafungulia mashtaka wawili hao ambao walihudumu katika serikali ya Kanali Gadafi, na mashtaka hayo yanajumuisha mauaji wakati Muamar Gadaffi alipoondolewa mamlakani kwa mapinduzi ya kiraia mwaka 2011.
Maafisa wa Libya wamekuwa wakitaka Saif kuhamishwa hadi Tripoli kutoka Zintan anakozuiliwa tangu akamatwe mwaka 2011.
Awali Seif alifikishwa mahakamani kwa muda kuhusiana na kesi nyingine anayokabiliwa nayo ya kutishia usalama wa nchi ambayo iliakhirishwa hadi Disemba.
No comments:
Post a Comment