Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Oganizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Oganizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo na Katibu wa Mwenyekiti, Abubakar Kitogo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Oganizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wakiandika taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wakiandika taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wakisikiliza na kuandika taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Oganizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo na kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF, Hamis Hassan.
Wapigapicha wa vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kusoma taarifa ya chama kuhusu kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF, Hamis Hassan.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kusoma taarifa ya chama kuhusu kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF, Hamis Hassan na kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Oganizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu chama hicho kulaani vitendo vya Naibu Spika, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwadhalilisha Wabunge wa upinzani, akiwemo Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Oganizesheni, Uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo.
VURUGU BUNGENI
- SERIKALI NA KITI CHA SPIKA WAJITIZAME UPYA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA
CUF Chama Cha Wananchi kinalaani vikali
kitendo cha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job
Ndungai, kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wabunge wa upinzani akiwemo Kiongozi wa
Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe.
Katika mjadala wa kupitisha muswada wa
mabadiliko ya sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 uliofanyika wiki
hii, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani alisimama kuomba kuongea. Kama ilivyo
utamaduni wa mabunge ya jumuiya ya madola, katika bunge kunakuwa na kambi mbili
na viongozi wawili katika kambi hizo. Viongozi hao wanawakilisha maoni ya pande
za serikali na upinzani na wana nafasi sawasawa katika kutaka ufafanuzi wa
jambo na kutoa ufafanuzi wa jambo. Kwa mfumo huo wa mabunge ya jumuiya ya
madola, kwa hapa Tanzania hivi sasa viongozi hao ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda
na Mhe. Freeman Mbowe ndiyo wanawakilisha maoni rasmi ya pande zote mbili na
kila wanaposimama pana umuhimu mkubwa Spika awape fursa ili waeleze hoja zao.
Kitendo cha Naibu Spika kumkataza Mhe.
Freeman Mbowe asiongee na kuamuru askari wamtoe bungeni kwa nguvu,
hakikubaliki. Ni kitendo cha aibu na hakikupaswa kufanywa na Naibu Spika wa
Bunge letu. Sisi CUF tunajiuliza, angesimama Mhe. Mizengo Pinda kuongea Naibu
Spika angemnyima nafasi? Na angethubutu kuamrisha Askari wamtoe nje? Kwa nini
haya yanatendwa na kiti cha Spika kwa mpinzani na hayawezi kutokea kwa kiongozi
wa serikali? Je Serikali ina mamlaka makubwa katika bunge kuliko Bunge lenyewe
hadi kiti cha spika kiendeshe masuala kwa taratibu za kupendelea serikali kwa
kadri ambavyo Spika ataona?
Muswada husika uliojadiliwa kwa dakika
90 ulikuwa na utata mkubwa, serikali imeubadili kwa nguvu na kuondoa maoni
muhimu ya wadau na pia upande wa Zanzibar haukushirikiswa ipasavyo na wajumbe
wa kamati ya sheria na katiba ya Bunge akiwemo Mhe. Tundu Lisu wamesisitiza
kuwa hawakupewa fursa ya kuchukua maoni kutoka kwa taasisi na watu muhimu
waliopo Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF upande wa
Zanzibar Mhe. Hamad Masoud ambaye pia ni mjumbe wa baraza la Wawakilishi
anathibitisha kuwa Zanzibar haikushirikishwa. Chama chetu cha CUF kina wabunge
wengi kutoka Zanzibar na wote wanasema hawakushirikishwa na hawana taarifa
ikiwa wananchi wao walishirikishwa. Je, kama hali ndiyo hii, tunatengeneza
katiba ya upande mmoja wa Nchi? Tunatengeneza katiba ya Tanganyika peke yake?
Njama za wazi za serikali na kiti cha
Spika kutelekeza maoni ya wananchi na kuyapatia kipaumbele yale ya CCM kwa
maslahi ya CCM, kunaondoa uhalali wa bunge na kiti cha spika katika kusimamia
mchakato huu. Moja ya njama za wazi ni ile ya wabunge 166 wa bunge la Katiba
wanaopaswa kupendekezwa na taasisi mbalimbali na kuteuliwa na Rais. Awali
waziri William Lukuvi alikijulisha chama chetu kuwa taasisi muhimu kama vyama
va siasa vyenye uwakilishi Bungeni vitatoa wabunge wa katiba watatu watatu kwa
kila chama na kwamba jambo hilo ndiyo msimamo wa serikali. CUF tumesikitishwa
na mabadiliko yaliyofanywa na lengo la CCM la kupitisha muswada unaompa mamlaka
ya uteuzi Rais kwani hivi sasa kila taasisi bila kujali uzito wa taasisi husika
itapaswa kuteua majina 9 na kumpa Rais na kisha Rais atateua jina moja au
hatateua kabisa jina lolote kutoka katika taasisi hiyo. Sheria hii inampa Rais
kuteua watu anaowataka kuwa wajumbe wa Bunge la kutunga katiba!
CCM na serikali yake wanajua kuwa
hujuma wanazozifanya katika mchakato wa katiba ndizo zitawapa katiba
wanayoitaka wao kama chama, hii ina maana kuwa katiba tunayoitengeneza
haitakuwa na uhalali wa wananchi, hii itakuwa ni katiba ya CCM.
Ombi la Wabunge wa CUF kuwa muswada huu
urudishwe kwa wananchi na kwa kamati kujadiliwa upya lilikuwa na mantiki kubwa.
Wabunge wa upinzani wote walioonesha msimamo wao kupinga muswada huu wanapaswa
kuungwa mkono na kila Mtanzania ambaye anahitaji tupate katiba ya Watanzania na
si ya CCM.
Kiti cha Spika kutaka kuwafunga midomo
wabunge wa Upinzani ni suala la hujuma kubwa. Mbunge mmoja Joseph Mbilinyi
alipigwa waziwazi na askari ndani ya bunge na kisha kutupwa kama mzigo nje ya
lango la bunge. Pamoja na kudhalilishwa huko kuna taarifa kuwa mbunge huyu
anasakwa na polisi na ametakiwa ajisalimishe polisi baada ya siku 2. Mhe. Mozza
Abeid Mbunge wa Viti Maalum wa CUF alivuliwa vazi lake la hijabu. Huu ni
udhalilishaji mkubwa wanawake usiokubalika. Haya yanatokea Tanzania ya leo,
inayotafuta katiba itakayotenda haki!
Naibu Spika alisikika mara kadhaa
akiwaamrisha askari wachukue hatua haraka na hata kiongozi wa askari wale
alipoenda hadi kwa spika na kuongea naye Spika alishikilia msimamo kuwa
kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni atolewe. CUF tunajiuliza, kiti cha
Spika na mawaziri na wabunge wa CCM wanafanya masuala haya kwa faida ya nani?
Na je wanadhani kulazimisha njama hizi mbaya ndiko kutatuelekeza kwenye katiba
bora ya wananchi?
Ni wazi watendaji serikalini wakiwemo
Mawaziri na Naibu Spika wanahujumu azma ya Rais Kikwete kukamilisha mchakato wa
kupata Katiba mpya. Ikumbukwe muswada wa kwanza wa Mabadiliko ya Katiba
uliopelekwa Bungeni ulikuwa mbovu sana na kwa hiyo ukachelewesha kwa maksudi
zoezi la kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya. Rais Kikwete alichukua hatua
ya kuzungumza na wapinzani ili kurekebisha muswada huo. Inaelekea watendaji
serikalini wakiwemo Mawaziri wanaendelea kumuhujumu Rais Kikwete asifanikishe
mchakato wa kupata katiba mpya.
Isitoshe Rais Kikwete na Tanzania kwa
ujumla inakabiliwa na changamoto za matamshi hasi yanayotolewa na viongozi na
asasi za Rwanda baada ya Rais Kikwete kuwapa ushauri wenye mantiki viongozi wa
Rwanda, Uganda na Kongo kuwa hali ya usalama ya Mashariki ya Kongo
itaimarika ikiwa Rwanda, Uganda na Kongo itazungumza na kufikia muafaka wa
kisiasa na waasi wao walioko Mashariki ya Kongo. Askari wa Tanzania wanashiriki
katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani Mashariki ya Kongo.
Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda wamekutana huku wakiitenga Tanzania
kuzungumzia ushirikiano wa kiuchumi unaopaswa kujadiliwa katika vikao vya
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ukizingatia changamoto ya Rwanda na
Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati huu ni muhimu kujenga umoja wa kitaifa.
Kitendo cha Naibu Spika cha kuamrisha askari wamtoe kwa nguvu Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya upinzani Bungeni kinahujumu uwepo wa umoja na mshikamano wa kitaifa
wakati Rais wetu amekuwa anakejeliwa na kutishwa na nchi jirani. Naibu Spika
anapaswa kuwa na mtazamo mpana na kuelewa changamoto zinazolikabili taifa letu.
Vitendo vyake vinamuhujumu Rais Kikwete katika azma yake ya kupata Katiba Mpya
na kukabiliana na changamoto za nchi jirani.
CUF inaendelea na juhudi ya kuwasiliana
na viongozi wa vyama vingine ili kuweka mkakati wa pamoja wa kukabiliana na
hujuma dhidi ya mchakato wa kupata katiba mpya na kuimarisha umoja wa kitaifa
katika kipindi hiki nyeti.
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba,
No comments:
Post a Comment