TANGAZO


Saturday, September 28, 2013

Serikali ya Tunisia iko tayari kujiuzulu


Wafuasi wa Ennahda chama kiliposhinda uchaguzi
Wakuu wa Tunisia wanasema serikali ya nchi inayoongozwa na chama cha Waislamu imekubali kujiuzulu katika majuma machache yajayo, baada ya kumalizika mazungumzo na upinzani usiokuwa wa kidini.
Serikali ya muda itachukua madaraka na kutayarisha uchaguzi mwengine.
Mazungumzo kuhusu namna ya kuunda serikali mpya yataanza Jumatatu.
Chama kikuu cha wafanyakazi wa Tunisia ndicho kilichopatanisha katika mazungumzo hayo baina ya chama tawala cha Ennahda na upinzani.

No comments:

Post a Comment